JINSI YA KUFUNGUA ACCOUNT UTT AMIS

Kama nilivyoombwa na wengi kuelezea hatua kwa hatua jinsi ya kufungua account kupitia UTT-AMIS na viambatanishi vyote unavyohitaji kukamilisha kazi hii.



Nitajaribu kufupisha maelezo sababu najua muda ni mali na usingependa kupoteza muda mwingi hapa kusoma badala yake uutumie muda wako vizuri katika kujiongezea maarifa yatakayokufaa maishani.


Kwanza kabisa UTT-AMIS ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, uliopo chini ya wizara ya fedha na mipango. Mfuko huu una zaidi ya mifuko mitano ndani yake yenye malengo tofauti tofauti kulingana na malengo ya mwekezaji. {Nitalieleza hili kwa mapana katika post zijaz}


Kwa leo nitaeleza jinsi ya kufungua account, kwanza kabisa kwa sasa UTT ili uweze kukamilisha kufungua account ni lazima ufike ofisini kwao. Office zao zipo kila kanda nchini Mwanza,Mbeya,Arusha, Dodoma na Dar.


Utahitajika kufika na viambatanisho vifuatavyo ili account yako iweze kukamilika, viambata hivyo ni pamoja na picha zako 2 passport size na kitambulisho kinachokubalika na serikali kama Nida,leseni au kile cha kura.


Baada ya kuwa ni vitu hivi fika ofisi ya UTT iliyo karibu na eneo lako na ndani ya muda mfupi utakua tayari umefanikiwa kufunguliwa account yako. Baada ya kufunguliwa accounnt mwambie aliyekuhudumia akuwekee App ya UTT kwenye simu yako. Hii itakusaidia kupata taarifa zote za account yako na utajionea mwenyewe fedha zako zinavyokua pindi tu unaponunua vipande. 


Kumbuka ukinunua vipande huwa inachelewa kwa siku 2 au tatu hadi kuonekana katika App yako hivyo ukiona unapitia changamoto hiyo usiwe na wasi wasi ni kwa muda mfupi tu na kila kitu kitakua sawa.


Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kununua hisa mtandanoni hatua kwa hatua

MFUKO WA UWEKEZAJI WA PAMOJA- UTT AMIS