Jinsi ya kununua hisa mtandanoni hatua kwa hatua
U hali gani mpenzi msomaji? Ni matumaini yangu u mzima wa afya..!
Pasi na kupoteza muda nikuelekeze jinsi ya kufanya manunuzi ya hisa mtandaoni au online kama wengi tulivyozoea kusema. Kwanza naamini unajua nini maana ya hisa na unajuza zinauzwa wapi, kwa Tanzania hisa zinauzwa ndani ya soko la Hisa Dar es Salaam au Dar es Salaam Stock Exchange kwa kifupi DSE. Zipo njia totauti tofauti za kuweza kufanya ununuzi wa hisa ila kwa leo nitaelezea njia ya mtandaoni kutumia simu yako au laptop hatua kwa hatua na hadi kufika mwisho kila msomaji atakua na uwezo wa kununua hisa akiwa nyumbani,kazini au popote.
Kwanza kabisa bonyeza NUNUA HISA itakupeleka moja kwa moja katika MTP ya DSE ambako utalog in ili uweze kuanza hatua za kununua hisa. Ili kufika hapa ni lazima uwe umeshafungua account account kwao DSE.
Bonyenza LOGIN (For investors who passed KYC) hapo utaletewa page ya wewe kuweka password ili uweze kuingia katika account yako. Utahitajika kuingiza kila kitu kama kinavyoonekana katika picha inayofuata ili uweze kuingaia kwenye account yako.
Baada ya kujaza kila kitu hivyo utabonyeza login. Itakupeleka moja kwa moja ndani ya account yako ya uwekezaji na hapo unaweza kuanza kufanya manunuzi mara moja bila kupoteza muda.
Baada ya kuingia utaona option znazoonekana upande wa kushoto, kwa kuwa tunaenda kununua bonyeza palipoandikwa BUY SHARES. Itakupeleka moja kwa moja hadi zinapoonekana share zote zilizo sokoni pamoja na bei zake. utaona idadi ya hisa ambazo zipo katika bei ya ofa na hapa unachotakiwa kufanya ni kuanza mchakato wa kununua kwa kubonyeza neno BUY upande wa kulia kwenye hisa za kampuni unayopenda kuinunu.
Nitabonyeza BUY kwa CRDB kama mfano ili uweze kuona kinachotokea. Baada ya kubonyeza buy italeta Popup window itakayoonekana hivi.Kufikia hapo itakua tayri umeweza kutengeneza order yako na moja kwa moja itakuhitaji kufanya malizpo ili order yako iweze kupelekwa sokoni na broker wako. Kwa njia ya simu unaweza kufanya malipo kwa urahisi kwa kuscan QR code au kutumia control number kama nitakavyoelekeza hapa chini.
Utabonyeza kwenye orders na kisha utaona order uliyoitengeneza itakua juu kabisa. kwa mwisho kulia kuna kialama cha risiti hivi bonyeza hapo kisha bonyeza View bill kama hivi
Ukiview bill utaletewa bill yako na kwa kutumia QR code unaweza kuscan na kufanya malipo direct ila pia unaweza kutumia control number kulipia kama malipo ya serikali na utakua umekamilisha ununuzi wako.
Kwa sababu leo nimekua nafanya kama mfano nitaonesha baada ya kulipia order yako itaonekana vipi katika accouunt yako. Nitatumia moja ya order zangu ambazo nimezifanya siku za nyuma ili kukuonesha mfano wa kitakavyoonekana uwe na picha halisi na usibabaike siku na wewe umeamua kununua kwa njia hii.
Hii ni order ya hisa 200 niliyoifanya January 2021 nikafanikiwa kununua hisa kwa shilingi 230 na hadi kufikia leo hisa moja ya CRDB imefika kiasi cha shilingi 430 unaweza kuona ongezeko la thamani katika uwekezaji huu. Hivyo nakuhimiza kama kijana mwenzangu jitume na uanze kuwekez leo, anza pole pole na baada ya muda utafika mbali sana.
Comments
Post a Comment