Posts

Showing posts from February, 2023

Umihimu wa kufanya utafiti kabla ya kufanya biashara au uwekezaji

Image
Ni muhimu sana kwako kufanya utafiti kabla huwekeza fedha zako katika eneo lolote lile. Hizi ni baadhi ya sababu zinazokulazimisha kufanya utafiti kabla ya kuwekeza. Uelewa mpana kuhusu uwekezaji  Kwa kufanya utafiti wako binafsi utapata uelewa mkubwa juu ya kile unachokitafiti kabla ya kuwekeza na hii itakusadia kupunguza hatari za kupoteza fedha zako lakini pia itakuongezea wigo mpana wa kutengeneza faida nzuri katika uwekezaji wako huo tarajiwa. Hapa itakufanya ufaye maamuzi sahihi ukiwa na uelewa mpana wa kila unachoenda kukifanya kabla hujaingia mzima mzima. Kukwepa matapeli Ulimwengu wa uwekezaji umejaa utapeli wa kila aina tena kwa miaka ya hivi sasa ambapo karibu kila huduma inaweza kupatikana mtandaoni. Kufanya utafiti wako binafsi itakusadia kuepikana na matapeli hawa na kulinda fedha zako ulizozipata kwa jasho na usingependa zipotee kwa aina njia rahisi kiasi hicho. Hata kama ni ndugu,jamaa au rafiki amekushirikisha fursa flani usipuuze kufanya utafiti wa kutosha kuhusu ...

Protect Your Money and Reach Your Financial Goals: The Importance of Doing Your Own Investment Research

Image
The Importance of Doing Your Own Research Before Investing Investing your money can be daunting, especially if you're new to the game. With so many options available, relying on others for advice and guidance can be tempting. However, it's important to remember that the ultimate decision about where to invest your hard-earned money should be made by you. This is why it's crucial to do your own research before making any investment decisions. In this blog post, we'll discuss why it's important to take the time to research your investments and what you can do to get started. Avoid Scams The investment world is full of scams and unethical schemes, and it's important to be aware of them. By doing your own research, you can learn about these scams and take steps to avoid them. This can help protect your money and ensure that your investments are safe. Some common scams to be aware of include Ponzi schemes, high-yield investment programs, and fake ICOs. Make Informed ...

JINSI YA KUFUNGUA ACCOUNT UTT AMIS

Image
Kama nilivyoombwa na wengi kuelezea hatua kwa hatua jinsi ya kufungua account kupitia UTT-AMIS na viambatanishi vyote unavyohitaji kukamilisha kazi hii. Nitajaribu kufupisha maelezo sababu najua muda ni mali na usingependa kupoteza muda mwingi hapa kusoma badala yake uutumie muda wako vizuri katika kujiongezea maarifa yatakayokufaa maishani. Kwanza kabisa UTT-AMIS ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, uliopo chini ya wizara ya fedha na mipango. Mfuko huu una zaidi ya mifuko mitano ndani yake yenye malengo tofauti tofauti kulingana na malengo ya mwekezaji. {Nitalieleza hili kwa mapana katika post zijaz} Kwa leo nitaeleza jinsi ya kufungua account, kwanza kabisa kwa sasa UTT ili uweze kukamilisha kufungua account ni lazima ufike ofisini kwao. Office zao zipo kila kanda nchini Mwanza,Mbeya,Arusha, Dodoma na Dar. Utahitajika kufika na viambatanisho vifuatavyo ili account yako iweze kukamilika, viambata hivyo ni pamoja na picha zako 2 passport size na kitambulisho kinachokubalika na serikali kam...

MFUKO WA UWEKEZAJI WA PAMOJA- UTT AMIS

Image
  Faida na hatari za uwekezaji katika mfuko wa pamoja  wa uwekezaji. Tuanze kuchambua faida zinazopatikana katika uwekezaji wa pamoja. Kutawanya hatari ya uwekezaji: Katika mfuko wa uwekezaji wa fedha huwekezwa kitaalam kwa katika sekta tofauti tofauti za uwekezaji kama hatifungani,Hisa na dhamana zingine za serikali au binafsi. Aina hii ya uwekezaji hupunguza hasara ikiwa moja ya sehemu mfuko ulipowekeza itatokea hasara. [soma zaidi post za nyuma]. Usimamizi wa Kitaalamu: Msimamizi wa mfuko aliye na ujuzi katika soko la fedha hufanya maamuzi ya uwekezaji kwa niaba ya wawekezaji wa mfuko husika. Hii inaweza kusababisha mapato ya juu ikilinganishwa na mtu anayefanya maamuzi ya uwekezaji bila kuwa na ujuzi wa anachokifanya. Pia, Uwekezaji katika mfuko wa pamoja humpa msimamizi wa mfuko uwezo wa kujadiliana na kudai riba kubwa kulingana kiwango kikubwa cha fedha zinazotarajiwa kuwekezwa, hivyo kuruhusu msimamizi wa mfuko kujadili fursa bora za uwekezaji na bei za dhamana. Hii ina...

Jinsi ya kununua hisa mtandanoni hatua kwa hatua

Image
 U hali gani mpenzi msomaji? Ni matumaini yangu u mzima wa afya..!  Pasi na kupoteza muda nikuelekeze jinsi ya kufanya manunuzi ya hisa mtandaoni au online kama wengi tulivyozoea kusema. Kwanza naamini unajua nini maana ya hisa na unajuza zinauzwa wapi, kwa Tanzania hisa zinauzwa ndani ya soko la Hisa Dar es Salaam au Dar es Salaam Stock Exchange kwa kifupi DSE. Zipo njia totauti tofauti za kuweza kufanya ununuzi wa hisa ila kwa leo nitaelezea njia ya mtandaoni kutumia simu yako au laptop hatua kwa hatua na hadi kufika mwisho kila msomaji atakua na uwezo wa kununua hisa akiwa nyumbani,kazini au popote. Kwanza kabisa bonyeza NUNUA HISA  itakupeleka moja kwa moja katika MTP ya DSE ambako utalog in ili uweze kuanza hatua za kununua hisa. Ili kufika hapa ni lazima uwe umeshafungua account account kwao DSE. Bonyenza LOGIN (For investors who passed KYC) hapo utaletewa page ya wewe kuweka password ili uweze kuingia katika account yako. Utahitajika kuingiza kila kitu kama kinavyo...