Umihimu wa kufanya utafiti kabla ya kufanya biashara au uwekezaji
Uelewa mpana kuhusu uwekezaji
Kwa kufanya utafiti wako binafsi utapata uelewa mkubwa juu ya kile unachokitafiti kabla ya kuwekeza na hii itakusadia kupunguza hatari za kupoteza fedha zako lakini pia itakuongezea wigo mpana wa kutengeneza faida nzuri katika uwekezaji wako huo tarajiwa. Hapa itakufanya ufaye maamuzi sahihi ukiwa na uelewa mpana wa kila unachoenda kukifanya kabla hujaingia mzima mzima.
Kukwepa matapeli
Ulimwengu wa uwekezaji umejaa utapeli wa kila aina tena kwa miaka ya hivi sasa ambapo karibu kila huduma inaweza kupatikana mtandaoni. Kufanya utafiti wako binafsi itakusadia kuepikana na matapeli hawa na kulinda fedha zako ulizozipata kwa jasho na usingependa zipotee kwa aina njia rahisi kiasi hicho. Hata kama ni ndugu,jamaa au rafiki amekushirikisha fursa flani usipuuze kufanya utafiti wa kutosha kuhusu habari ile kwani unaweza kujikuta unaanguka kwenye mikono ya matapeli na ikapelekea wewe na mwenzako mkajikuta mmepoteza fedha zenu kwa uzembe mkubwa.
Kufanya maamuzi yaliyojitosheleza
Pale unapotegemea watu wengine wakueleze ni wapi unahitaji kuwekeza fedha zako ni dhahiri kwamba hujawa tayari kuianza safari ya uhuru wa kifedha. Hii ni kwa sababu huwezi kuandesha maisha yako ya kifedha na kufikia malengo makubwa kama hujui kwa nini ulifanya maamuzi flani na badala yake unajua tu nilisaidiwa na mtu X kufanya ABC. Kwa kufanya utafiti wako itakuasaidia kufanya maamuzi yako binafsi yenye kushabihiana na malengo yako.
Kuwa rubani
Uwekezaji unaweza kuwa mgumu sana ila unapofanya maamuzi yako mwenyewe inakusadia kuwa kiongozi wa maamuzi yako ya uwekezaji na kifedha. unakua katika nafsi nzuri ya kuelewa mabonde na mlilima ya soko la uwekezaji na unauwezo wa kufanya maamuzi sahihi kulingana na taarif sahihi unazokua umekusanya.
Uhuru
Kufanya utafiti wako inakusadia kuwa huru na kutokua tegemezi kwa mtu yeyote, na pia inakulainishia kufanya maamuzi kulingana na malengo ya muda mrefu uliyojiwekea. Vile vile huwezi kuumia moyoi endapo utapata hasara katka uwekezaji wako sababu unajua A to Z ya kwa nini uliamua kufanya maamuzi yale na nini kilikusukuma kufika pale. Kwa kifupi huna wakumlaumu kwa maamuzi uliofanya peke yako.
Kuhitimisha ni muhimu kufanya utafiti wa kina kabla hujawekeza au kufanya biashara ya aina yeyote kama kweli unahitaji mafanikio. Ukiwa mvivu kufanya tafiti hizi ujue kabisa unajiandaa kupata hasara katika kile unachoenda kukifanya.
Comments
Post a Comment